Xi Jinping ametoa hotuba muhimu kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) uliofunguliwa leo hapa Beijing.
Kwenye hotuba yake, Xi amesema, kuanzia sasa jukumu kuu la CPC ni kuongoza wananchi wa makabila mbalimbali nchini China kujenga nchi ya kisasa ya kijamaa katika pande zote, na kutimiza lengo la pili la miaka mia moja, ili kusukuma mbele ustawishaji wa taifa la China kwa njia ya China .
Xi amesema, China inafuata sera za diplomasia ya amani ya kujitawala na kujiamulia . Amesema siku zote China inaamua msimamo na sera zake kufuatia hali halisi, kulinda kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa na haki duniani, na inapinga kithabiti aina yoyote ya umwamba na siasa ya kinguvu, pia inapinga wazo la Vita Baridi, vitendo vya kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kupinga vigezo viwili. Amesisitiza kuwa, China haitafanya umwamba, wala haitavamia nchi nyingine daima.
Amesema, China imekuwa mshirika mkubwa wa kibiashara wa nchi na sehemu zaidi ya 140, na inashika nafasi ya kwanza duniani kwa thamani ya biashara ya bidhaa. Pia Xi amesema, China inashika nafasi ya kwanza katika kuvutia uwekezaji wa nje na kutoa uwekezaji kwa nchi za nje, na imeendeleza sera ya kufungua mlango kwa nje kwa upana na kina zaidi.
Aidha, Xi amesema, China itasukuma mbele kwa hatua madhubuti na tulivu kuufanya utoaji wa hewa chafu kufikia kilele halafu kutimiza usawa wa utoaji na ufyonzaji wa hewa hiyo. Pia amesema, China itashiriki kwenye usimamizi wa kimataifa wa juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.