Jukumu kuu la CPC ni kutimiza lengo la pili la miaka mia moja
2022-10-16 12:36:05| CRI

Xi Jinping alipohutubia Mkutano Mkuu wa 20 wa Wajumbe Wote wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) uliofunguliwa leo hapa Beijing amesema, kuanzia sasa jukumu kuu la CPC ni kuongoza wananchi wa makabila mbalimbali nchini China kujenga nchi ya kisasa ya kijamaa katika pande zote, na kutimiza lengo la pili la miaka mia moja, ili kusukuma mbele ustawi wa taifa la China kwa njia ya kichina.