Kuwatafutia wananchi neema na furaha ni lengo lisilobadilika la Chama cha Kikomunisti cha China
2022-10-17 10:48:26| CRI

Mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ulifunguliwa rasmi Oktoba 16 hapa Beijing, na Xi Jinping alitoa hotuba kwenye mkutano huo kwa niaba ya kamati kuu ya 19 ya CPC.

Katika hotuba yake neno “Wananchi” ni neno lililotajwa mara nyingi zaidi. Iwe ni kwenye majumuisho ya mafanikio yaliyopatikana katika muongo uliopita, iwe ni kwenye mpango wa kazi kwa siku za baadaye, yote yameonesha dhamira thabiti ya CPC ya kuwatafutia wananchi neema na furaha, na kulitafutia taifa ustawishwaji mpya na kuonesha moyo wa viongozi wakuu wa China wa kuwajali wananchi.

Wakati wa majumuisho ya kazi zilizofanywa katika muongo uliopita, Rais Xi amesema katika miaka kumi iliyopita, watu wa China wameshuhudia mambo makubwa matatu yenye umuhimu mkubwa katika zama hii na historia kwa Chama na wananchi: kwanza ni kutimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwa CPC; pili ni Ujamaa wenye umaalum wa China kuingia kwenye zama mpya; tatu ni kukamilisha jukumu la kihistoria la kutokomeza umaskini uliokithiri na kukamilisha ujenzi wa Jamii yenye Maisha Bora, na hivyo kufikia Lengo la Kwanza la Miaka 100.

Amesema huu ni ushindi wa kihistoria uliopatikana kwa juhudi za pamoja za Chama na wananchi, ni ushindi wa kihistoria unaong’ara kwenye historia ya maendeleo ya taifa la China, na pia ni ushindi wa kihistoria wenye athari za kina kwa dunia nzima, ushindi ambao umewapatia wananchi zaidi ya bilioni 1.4 wa China hisia za mafanikio, furaha na usalama.