China yashikilia ufunguaji mlango wenye kiwango cha juu
2022-10-17 16:20:46| cri

Mkutano Mkuu wa 20 wa Wajumbe Wote wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umefunguliwa mjini Beijing, ambapo Xi Jinping akitoa hotuba kwa niaba ya Kamati Kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China ameeleza kuwa, China itafanya juhudi kuhimiza maendeleo ya hali ya juu, na kushikilia ufunguaji mlango wenye kiwango cha juu.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa, kuanzia sasa China imeanza safari mpya ya kujenga nchi ya kisasa ya kijamaa katika pande zote, na jukumu muhimu ni kuhimiza maendeleo ya hali ya juu. Pia imesema China itaongeza msukumo wa mzunguko wa ndani, kuinua kiwango cha mzunguko wa kimataifa, na kuharakisha ujenzi wa mfumo wa kisasa wa uchumi.

Hivi sasa, thamani ya jumla ya uchumi wa China inachukua asilimia 18.5 ya uchumi wa dunia, ikishika nafasi ya pili duniani, Pato la Taifa kwa kila mtu linazidi dola za kimarekani elfu 10, idadi ya watu wenye pato la kati imezidi milioni 400, ambayo ni kubwa zaidi duniani. China imekuwa mshirika mkubwa wa kibiashara wa nchi na sehemu zaidi ya 140, na inashika nafasi ya kwanza duniani kwa thamani ya biashara ya bidhaa, na pia inashika nafasi za mwanzo katika kuvutia uwekezaji wa nje na kutoa uwekezaji kwa nchi za nje.