Xi Jinping ashiriki kwenye mjadala wa wajumbe wa mkoa wa Guangxi wanaohudhuria mkutano mkuu wa 20 wa wajumbe wote wa Chama cha CPC
2022-10-17 16:18:51| cri

Xi Jinping leo hapa Beijing ameshiriki kwenye mjadala wa wajumbe wa mkoa wa Guangxi wanaohudhuria mkutano mkuu wa 20 wa wajumbe wote wa Chama cha Kikomunisiti cha China CPC.

Xi amesisitiza kuwa mkutano huo wa chama cha CPC umeweka bayana mwelekeo wa kusonga mbele wa shughuli za chama na taifa, ambao ni azimio la kisiasa na mwongozo wa hatua wa chama kuongoza watu wa makabila mbalimbali kushikilia na kuendeleza ujamaa wenye umaalumu wa China katika safari na zama mpya. Ili kujifunza na kutekeleza moyo wa mkutano mkuu wa 20 wa wajumbe wote wa chama cha CPC, tunatakiwa kushikilia kithabiti maana pana ya kazi za miaka mitano iliyopita na mageuzi makubwa ya zama mpya katika miaka 10 iliyopita, mtazamo na mbinu za fikra ya ujamaa wenye umaalumu wa China, kusukuma mbele jukumu tukufu la ustawi wa taifa la China kwa njia ya kisasa ya kichina, matakwa muhimu ya mapinduzi matukufu ya jamii yanayoongozwa na mageuzi matukufu ya binafsi, na matakwa ya zama ya juhudi na mshikamano.

Wajumbe watano wa mkoa wa Guangxi wametoa maoni kuhusu ripoti, wakitoa hotuba kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo utandawazi wa kisasa wa kichina wa Guangxi, kuimarisha mwamko wa kujenga jumuiya ya taifa la China, kuhifadhi mazingira ya mji wa Guilin, kuendeleza shughuli za kilimo na kuendelea kuimarisha uvumbuzi.