Viongozi wa vyama na serikali za nchi za Afrika wapongeza kufanyika kwa mkutano mkuu wa 20 wa CPC
2022-10-17 09:14:03| CRI

Mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC ulianza jana mjini Beijing, huku viongozi wa vyama vya kisiasa vya nchi mbalimbali za Afrika wakitoa salamu za kupongeza kufanyika kwa mkutano huo, kwa kamati kuu ya CPC na kwa katibu mkuu wake Xi Jinping.

Mwenyekiti wa chama cha ANC cha Afrika Kusini ambaye pia ni Rais wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa, amesema mkutano mkuu wa 20 wa  CPC unafanyika wakati hali ya dunia inashuhudia mabadiliko makubwa. Chama cha ANC kinathamini urafiki wa kindugu na CPC, na mshikamano na mitazamo sawa kuhusu thamani ni msingi imara wa uhusiano kati ya vyama viwili. Amesema ana imani kuwa vyama hivi viwili vitatumia vyema fursa, kukabiliana na changamoto kwa pamoja ili kukuza uhusiano wao. Ameeleza matumaini yake kuwa mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha CPC utapata matunda ya kiujenzi, kuendelea kupanua na kukuza Chama cha CPC ili iongoze watu wote wa China kuelekea kwenye ustawi wa pamoja.

Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon amepongeza kufanyika kwa mkutano mkuu huo, akiamini kuwa mkutano huo utafanya maamuzi sahihi na yenye busara. Ameipongeza CPC kwa kuifanikisha China kuwa moja ya nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani na kuleta utulivu na ustawi kwa watu wa China.

Naye naibu mwenyekiti na katibu mkuu wa chama cha Ustawi cha Ethiopia Bw. Adem Farah, amesema chini ya uongozi imara na wenye busara wa katibu mkuu Xi Jinping, China imeanza safari ya kutimiza ustawishwaji mpya wa taifa na kuanzisha mtindo mpya wa maendeleo ya binadamu.