Tanzania yatoa tahadhari kuhusu uwezekano wa mlipuko wa kipindupindu
2022-10-18 08:00:47| CRI

Mamlaka za afya nchini Tanzania zimetoa tahadhari kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kufuatia nchi jirani ya Malawi kutangaza mlipuko wa ugonjwa huo.

Mamlaka nchini Malawi zimetangaza kuwa ugonjwa wa kipindupindu umeenea kwenye wilaya 25, na kusababisha vifo vya watu 132 na kuwaathiri wengine 4,604.

Mganga mkuu wa serikali ya Tanzania Bw. Aifello Sichalwe amewataka wananchi kuzingatia hatua za udhibiti wa mlipuko huo, na kumpeleka hospitali mtu yeyote anayeshukiwa kukumbwa na ugonjwa huo.