Ujenzi wa mambo ya kisasa wenye umaalum wa China watoa chaguo jipya kwa binadamu kutimiza lengo hilo
2022-10-18 09:26:38| CRI

Kwenye Mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) uliofunguliwa rasmi Oktoba 16 hapa Beijing, Xi Jinping alitoa hotuba kwa niaba ya Kamati Kuu ya 19 ya CPC. Kwenye hotuba yake, Xi ameweka mpango wa kimkakati kuhusu kuijenga China kuwa nchi ya kisasa ya kijamaa kwa pande zote, na kufafanua umaalum muhimu na matakwa ya kimsingi ya ujenzi huo, hotuba ambayo imefuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa.

Xi amesisitiza kuwa ujenzi wa nchi ya kisasa kwenye umaalum wa China ni ujenzi wa nchi ya kisasa ya kijamaa chini ya uongozi wa CPC, ambao si kama tu una sifa za pamoja kama nchi mbalimbali za kisasa, bali pia una umaalumu wake unaolingana na hali halisi ya China. Amesema, ujenzi wa nchi ya kisasa kwenye umaalum wa China ni ujenzi wa mambo ya kisasa unaohusisha idadi kubwa ya watu, unaolenga kuleta ustawi wa pamoja kwa wananchi wote, yenye masikilizano kati ya ustaarabu wa kimali na kiroho, yenye mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili, na unaoelekea kwenye amani na maendeleo.

Mafanikio yaliyopatikana kwenye ujenzi wa nchi ya kisasa yenye umaalum wa China yamedhihirisha kuwa ujenzi wa mambo ya kisasa sio hataza ya nchi za magharibi, na kila nchi inaweza kupiga hatua kubwa kimaendeleo endapo itafuata njia inayofaa hali yake halisi.

Ujenzi wa nchi ya kisasa wenye umaalum wa China unasisitiza “kufuata njia ya amani ya kutimiza maendeleo”, kupendekeza kuingiliana na kufundishana kati ya staarabu tofauti, kuvunja “nadharia ya mgongano kati ya staarabu” iliyotungwa na nchi za magharibi, kuvumbua mtindo mpya ulio shirikishi wa ustaarabu wa binadamu, na kuhimiza amani na maendeleo ya dunia nzima.