Marais wa China na Uganda wapongezana kwa maadhimisho ya miaka 60 tangu zianzishe uhusiano wa kibalozi
2022-10-18 15:11:02| cri

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni wamepongezana kupitia simu kwa kuadhimisha miaka 60 tangu nchi hizi mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi.

Rais Xi amesema, urafiki wa jadi kati ya China na Uganda una historia ndefu. Katika miaka ya hivi karibuni, nchi mbili zimeanzisha uhusiano wa ushirikiano na wa kiwenzi wa pande zote, maelewano ya kisiasa yanazidi kuimarishwa, ushirikiano wa sekta mbalimbali unaendelea kuzidishwa. Nchi hizo mbili zinaungana kithabiti katika masuala muhimu yanayofuatiliwa na pande mbili na yanayohusu maslahi ya upande mwingine, na kushirikiana vizuri katika mambo ya kikanda na kimataifa.

Ameongeza kuwa anatilia maanani kuendeleza uhusiano kati ya China na Uganda, na anapenda kufanya juhudi pamoja na rais Museveni kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali chini ya ujenzi wa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na utaratibu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, ili kunufaisha nchi mbili na watu wake na kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.

Kwa upande wa rais Museveni, amesema kuwa tangu Uganda na China zianzishe uhusiano wa kibalozi katika miaka 60 iliyopita, nchi hizo mbili zimefanya uratibu na ushirikiano kwa karibu, na kusukuma mbele ushirikiano mwingi muhimu, huku uhusiano kati ya nchi mbili ukiwa na uhai siku zote. Uganda itaendelea kufanya juhudi kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati yake na China.