Serikali ya Ethiopia yapanga kuanza tena utoaji wa misaada ya kibinadamu na huduma kwenye maeneo yaliyokamatwa Tigray
2022-10-19 08:36:07| CRI

Serikali ya Ethiopia imesema maandalizi yanaendelea ili kuanza tena utoaji wa misaada ya kibinadamu na huduma kwenye maeneo yaliyokamatwa hivi karibuni katika eneo la Tigray.

Taarifa iliyotolewa na serikali inasema Jeshi la Ethiopia limetwaa udhibiti wa miji ya Shire, Alamata na Korem, na kuvisukuma vikosi vya waasi wa Tigray.

Taarifa imesema serikali ya Ethiopia inafanya maandalizi muhimu na itafanya uratibu na mashirika ya kibinadamu ili kutoa misaada ya kibinadamu kupitia maeneo yanayoshikiliwa na jeshi la serikali, ikiwa ni pamoja na kupitia uwanja wa ndege wa Shire.

Taarifa pia imesema kutokana na umakini mkubwa wa jeshi la taifa, jeshi hilo limefanikiwa kuwalinda raia, na kuepuka hali mbaya iliyokuwa imetabiriwa kwenye kauli za kundi la waasi la TPLF.