Sudan yatangaza kuunga mkono uamuzi wa OPEC+ kuhusu kupunguza uzalishaji wa mafuta
2022-10-19 09:05:16| CRI

Sudan imetangaza kuunga mkono uamuzi wa Jumuiya ya Nchi Zinazozalisha Mafuta Duniani na washirika wake OPEC+ kuhusu kupunguza uzalishaji wa mafuta.

Wizara ya mambo ya nje ya Sudan imetoa taarifa ikisema Sudan ikiwa ni mwanachama wa jumuiya hiyo, inasisitiza kuwa uamuzi wa kupunguza uzalishaji wa mafuta ni maelewano ya nchi zote wanachama wa jumuiya hiyo.

Taarifa hiyo inasisitiza uungaji mkono wa Sudan kwa msimamo wa Saudi Arabia kwamba uamuzi huo ulitolewa kwenye msingi wa uchumi, na unalenga kudumisha uwiano wa usambazaji na mahitaji katika soko la mafuta, pamoja na kupunguza mabadiliko yasiyoendana na maslahi ya watumiaji na wazalishaji.