Vifo kutokana na Ebola nchini Uganda vyaongezeka hadi 24
2022-10-19 08:34:18| CRI

Wizara ya afya ya Uganda imetangaza kuwa idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa Ebola imeongezeka hadi kufikia 24, baada ya watu watano kuripotiwa kufa kwa ugonjwa huo katika siku nne zilizopita.

Wizara hiyo pia imesema idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa pia imeongezeka hadi 60, idadi ya waliopona imefikia 24, na idadi ya watu waliolazwa ni 11.

Serikali imeweka zuio la siku 21 na kutekeleza marufuku ya kutotoka nje wakati wa usiku kwenye wilaya za Mubende na Kassanda ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo. Serikali pia imeuweka mji wa Kampala kwenye tahadhari kama maambukizi yatatokea katika mji huo.