Kijiji cha vielelezo vya ushirikiano kati ya China na Afrika katika kukuza kilimo na kupunguza umaskini chazinduliwa Kenya
2022-10-19 08:59:13| CRI

Kijiji cha kwanza cha vielelezo vya ushirikiano kati ya China na Afrika katika kukuza kilimo na kupunguza umaskini kimezinduliwa katika kijiji cha Matangi Tisa, kaunti ya Nakuru nchini Kenya, kikiwa ni moja ya vijiji vya vielelezo  vya kwanza kuzinduliwa na Jumuiya ya Ushirikiano wa  Kusini-Kusini wa Elimu ya Kilimo na Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, BRASSCAL.

 Naibu mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Nanjing, China Bw. Hu Feng alipohutubuia shughuli hiyo kupitia video, alisema anatarajia kijiji hicho kitakuwa mfano wa kuigwa na kutimiza lengo la kupunguza umaskini na kunufaisha wakulima kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kilimo kutoka China, ikihimiza kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakbali wa pamoja ya kiwango cha juu .

Katika shughuli hiyo  naibu mkuu  wa Chuo Kikuu cha Egerton, Bw. Richard Mulwa alieleza nia ya kutaka ushirikiano wa kiwenzi na kimkakati kati ya chuo hicho na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Nanjing uwe karibu zaidi kupitia kuanzishwa kwa kijiji hicho cha vielelezo.