Mshauri maalumu wa UM aeleza wasiwasi juu ya mapigano yaliyoibuka tena Tigray, Ethiopia
2022-10-20 09:05:51| CRI

Mshauri maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia kuzuia mauaji ya kimbari Bi. Alice Wairimu Nderitu, ameeleza wasiwasi wake kuhusu mapigano yaliyoibuka tena katika eneo la Tigray nchini Ethiopia na kutaka yasitishwe mara moja, na kuitaka serikali ya Ethiopia na mamlaka ya Tigray kuchunguza na kuwafikisha mbele ya sheria waliokiuka vibaya haki za binadamu.

Bi. Nderitu amesema kuwalenga raia kwa msingi wa makabila au uhusiano wao na pande zilizoshiriki katika vita, bado ni sifa kuu ya mgogoro huo, na viwango vya kutisha vya kauli za chuki na uchochezi zimezidisha mgogoro huo.