Demokrasia ya umma kwenye mchakato kamili yahakikisha watu wa China wanajiamulia mambo ya taifa
2022-10-20 09:06:46| CRI

Mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ulifunguliwa Oktoba 16 hapa Beijing, Bw. Xi Jinping alipotoa hotuba kwenye mkutano huo kwa niaba ya Kamati kuu ya 19 ya Chama, alifafanua kwa pande zote sifa na manufaa ya demokrasia ya umma kwenye mchakato kamili, na kuonesha mwelekeo kwa China kuendeleza siasa ya demokrasia ya kijamaa katika zama mpya. Hotuba hiyo pia imefungua dirisha muhimu kwa jumuiya ya kimataifa kuangalia ubora wa demokrasia nchini China.

Bw. Xi Jinping amesema, demokrasia ya umma ni uhai wa ujamaa, na pia ni sifa inayotakiwa katika kujenga kwa pande zote nchi ya kisasa ya kijamaa. Kwa upande wa uhakikisho wa kimfumo, Bunge la Umma ni chombo chenye umuhimu wa kimfumo wa kufanikisha demokrasia ya umma kwenye mchakato kamili, na mfumo wa mashauriano ya kisiasa ni mfumo maalumu na wa kipekee wa siasa ya demokrasia ya kijamaa nchini China.

Katika muongo uliopita toka kutokomeza umaskini uliokithiri, hadi kukamilisha ujenzi wa Jamii yenye Maisha Bora, hadi kuanza safari mpya ya kujenga kwa pande zote nchi ya kisasa ya kijamaa na kuelekea kwenye lengo la kutimiza ustawi wa pamoja, demokrasia ya umma kwenye mchakato kamili imeonesha uchangamfu mkubwa na nguvu kubwa ya uhai.

Mfumo wa demokrasia kamwe hautakiwi kuwa wa aina moja tu dunia nzima. Ni ule mfumo wa demokrasia unaojikita kwenye nchi na kufaa hali halisi ya taifa, ndio unaotegemeka na kutekelezeka. Kwenye safari mpya ya kujenga kwa pande zote nchi ya kisasa ya kijamaa, CPC kitaendelea kukuza demokrasia ya umma kwa mchakato kamili, kuhakikisha wananchi wanajiamulia mambo ya taifa, na kutoa mchango wa China kwenye kurutubisha na kuendeleza ustaarabu wa kisiasa wa binadamu.