Rais wa Tanzania atoa wito wa utungaji wa sheria za kuwawezesha wanawake
2022-10-21 08:55:52| CRI

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania ametoa wito wa kupitishwa sheria zinazolenga kuwawezesha wanawake.

Akiongea mjini Dar es salaam kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Wanawake kwenye Sheria na Maendeleo barani Afrika (WiLDAF), Rais Samia amesema Tanzania inahitaji sheria zitakazohakikisha ushiriki kamili wa wanawake kwenye shughuli za uchumi na umiliki wa raslimali za nchi.

Taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania imesema takwimu zinaonesha kuwa idadi kubwa ya wanawake wanashiriki kwenye shughuli za maendeleo ya kiuchumi, lakini baadhi ya mila zinakwamisha wanawake kunufaika na matunda ya maendeleo.

Amesema kupitishwa kwa sheria hizo kutawalinda wanawake dhidi ya vizuizi kandamizi vilivyokuwepo kwa muda mrefu.