Mashirika ya kibinadamu ya UM yataka kuongeza msaada kwa Somalia
2022-10-21 08:58:04| CRI

Mashirika ya misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yamesema mahitaji yanayoongezeka kwa kasi nchini Somalia kutokana na ukame mkali, yamelazimisha kuongezeka kwa misaada kuliko ilivyopangwa katika lengo la mwezi Januari.

Kwa mujibu wa Ofisi ya uratibu wa masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA, Mpango wa Mwitikio wa Kibinadamu wa mwaka 2022 sasa unawalenga watu milioni 7.6, ikiwa ni ongezeko la asilimia 40 tangu Januari, kwa kutumia dola za kimarekani bilioni moja zilizotolewa na wafadhili hadi sasa kwa mwaka huu.

OCHA imesema kutokana na hali ya ukame kuzidi kuwa mbaya, dola za kimarekani bilioni moja za ziada zitahitajika ili kutoa msaada wa kuokoa maisha ifikapo mwisho wa Disemba na mwanzoni mwa mwaka kesho.