China inayofuata njia ya amani ya kutafuta maendeleo ni fursa kwa dunia
2022-10-21 10:22:21| CRI

"China siku zote imekuwa ikifuata kanuni ya sera ya mambo ya nje ya kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo ya pamoja, na kujitolea kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja." Mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC unaendelea kufanyika hapa Beijing, na kauli hii iliyotolewa na Bw. Xi Jinping alipouhutubia mkutano huo imeibua mjadala mkubwa katika jumuiya ya kimataifa. Wachambuzi wanaona hii inaonyesha azma na imani ya China ya kufuata njia ya kisasa ya kutafuta maendeleo ya amani, na kwamba Chama cha Kikomunisti cha China "kitaendelea kutoa mchango mkubwa zaidi kwa amani, maendeleo na ustawi wa dunia."

 

Katika miongo michache tu iliyopita, China imekamilisha mchakato wa mapinduzi ya kiviwanda ambao nchi zilizoendelea zimepitia kwa mamia ya miaka, na kufanikisha miujiza miwili ya maendeleo ya kasi ya uchumi na utulivu wa muda mrefu wa kijamii. Haya ni matokeo ya kazi kubwa ya watu wa China wakiongozwa na Chama cha Kikomunisti cha China, na pia ni kwa sababu chama tawala cha China siku zote kimekuwa kikifahamu mwelekeo wa maendeleo ya jumla wa zama na kuzingatia njia ya maendeleo ya amani.

 

Kufuata njia ya maendeleo ya amani sio tu kunawezesha China kupiga hatua kubwa kuelekea kuwa nchi ya kisasa, bali pia kuingiza nguvu chanya kubwa kwa amani na maendeleo ya dunia. China siku zote imekuwa ikichukua hatua madhubuti kulinda amani ya dunia na kukuza maendeleo ya pamoja.

 

 "Kulinda kanuni za kimsingi za mahusiano ya kimataifa, kulinda usawa na haki ya kimataifa", "Kukuza ujenzi wa uchumi wa dunia ulio wazi", "Kuzingatia utaratibu halisi wa pande nyingi", "China haitafuti umwamba na kamwe haitatafuta kupanua ardhi yake"... ni chaguo la China na dhana thabiti inayotekelezwa kivitendo na China.

 

“Nchi tulivu huwa ni tajiri, lakini nchi yenye machafuko huwa ni maskini". Amani ni msingi wa maendeleo, na maendeleo ni uhakikisho wa amani. Kwa sasa, China inaelekea kujijenga kuwa nchi kubwa ya kisasa ya kijamaa kwa pande zote na kutimiza lengo lake la pili la miaka 100. Ripoti aliyotoa Xi imesema, "China inafuata sera ya msingi ya kitaifa ya kufungua mlango, inafuata kithabiti mkakati ulio wazi wa kusaidiana na kunufaishana, na maendeleo mapya ya China yatakuwa fursa mpya kwa dunia." Hii ina maana kwamba chini ya mwongozo wa mpango mpya wa maendeleo, China na dunia zitaunda maingiliano mazuri zaidi.