Dhamira ya China ya kusukuma mbele ufunguaji mlango wa kiwango cha juu haitabadilika
2022-10-21 08:59:09| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin amesisitiza kuwa China itaendelea kusukuma mbele ufunguaji mlango kwa kiwango cha juu, na dhamira yake ya kujenga mazingira ya kibiashara yanayofuata kanuni za soko, usimamizi wa kisheria na viwango vya kimataifa haitabadilika.

Msemaji huyo amesema kufungua mlango ni sera ya msingi ya China, na pia ni sifa dhahiri ya China ya leo. Tangu mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ufanyike, China imekuwa ikitekeleza kithabiti mkakati wa kufungua mlango na kujenga hali mpya ya ufunguaji mlango kwa pande zote, katika ngazi nyingi na kwenye nyanja mbalimbali.

Bw. Wang Wenbin amesema ingawa sintofahamu kuhusu ufufukaji wa uchumi wa dunia imeongezeka kutokana na mabadiliko makubwa yanayoshuhudiwa katika hali ya kimataifa, lakini mwelekeo wa uchumi wa China wenye ustahimilivu mkubwa na mustakbali mzuri hautabadilika.