Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC wafungwa Beijing
2022-10-22 13:10:41| CRI

Mkutano Mkuu wa 20 wa chama tawala cha China Chama cha Kikomunisti cha China CPC uliofanyika kwa siku 7 umefungwa leo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.

Mkutano huo umechagua Kamati Kuu ya 20 ya CPC na Kamati Kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu, kupitisha azimio kuhusu ripoti ya kazi ya Kamati Kuu ya 19 ya CPC, kupitisha azimio kuhusu ripoti ya kazi ya Kamati Kuu ya 19 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC, na azimio kuhusu marekebisho ya katiba ya CPC.

Mkutano mkuu wa CPC na kamati kuu iliyochaguliwa na mkutano huo ni vyombo vikuu vya uongozi vya CPC. Mkutano Mkuu wa CPC unafanyika kila baadaya miaka mitano.