Kikao cha kwanza cha wajumbe wote cha Kamati Kuu ya 20 ya CPC chafanyika Beijing
2022-10-23 13:28:30| CRI

Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC ambacho ni chama tawala nchini, imeitisha kikao chake cha kwanza cha wajumbe wote leo Jumapili hapa Beijing. Kikao hicho kimechagua wajumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya CPC, wajumbe wa kamati ya kudumu ya ofisi ya siasa ya kamati kuu ya CPC, na katibu mkuu wa kamati kuu ya CPC. Xi Jinping aliendesha kikao hicho na kutoa hotuba muhimu baada ya kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa kamati kuu ya CPC.

Waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na wajumbe 203 wa Kamati Kuu ya CPC na wajumbe mbadala 168. Wajumbe wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu pia walishuhudia kikao hicho.

Kikao hicho kimepitisha wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC waliopendekezwa na kamati ya kudumu ya ofisi ya siasa ya Kamati Kuu ya CPC; kuamua wajumbe wa kamati kuu ya jeshi; kuidhinisha majina ya katibu, manaibu wake na wajumbe wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu waliochaguliwa kwenye kikao cha kwanza cha wajumbe wote wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu.