Tanzania yahamasisha wazimamoto zaidi ya 600 kuzima moto katika Mlima Kilimanjaro
2022-10-24 09:38:54| CRI

Mamlaka za Tanzania zimewahamasisha wazimamoto zaidi ya 600 kuzima moto katika Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika.

Akiongea na shirika la habari la China Xinhua kwenye mahojiano ya simu, mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amesema wazimamoto wametoka katika kikosi cha Zimamoto na Uokozi cha Tanzania, Mbuga za Taifa, polisi, skauti, wanamgambo na sekta binafsi.

Babu amesema moto huo ulizuka Ijumaa usiku katika urefu wa mita 4,000 kutoka usawa wa bahari upande wa kusini mwa mlima na kusambaa haraka kutokana na upepo mkali. Amebainisha kuwa chanzo cha moto na hasara bado haijajulikana. Awali alisema walikuwa na mpango wa kuita Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ili kusaidia kuzima moto lakini mpango huo ulitupiliwa mbali baada ya ripoti kuonesha kuwa kuna maendeleo mazuri katika kuzima moto.