China kuanza safari mpya na kutoa fursa mpya kwa dunia
2022-10-24 14:38:55| CRI

Wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya Kisiasa ya awamu mpya ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) jana wamekutana na waandishi wa habari wa ndani na nje ya China.

Kwenye mkutano huo Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CPC amesisitiza kuwa, katika zama mpya, China itatimiza maisha bora zaidi kwa wananchi wake, na kutoa fursa mpya kwa dunia nzima. Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) limetoa tahariri inayozungumzia safari mpya ya China na kutoa fursa mpya kwa dunia.

Tahariri hiyo inasema, ili kuelewa China ya leo, ni lazima kuelewa CPC kwanza. Mkutano Mkuu wa 20 wa Wajumbe Wote wa CPC uliomalizika hivi karibuni umeonesha mwelekeo wa kutimiza lengo la pili la miaka mia moja la China katika zama mpya na safari mpya, kuamua mwongozo wa hatua, na pia kutoa fursa muhimu kwa jamii ya kimataifa kuelewa utawala wa CPC nchini China.

China haiwezi kujiendeleza bila ya dunia, na dunia pia inaihitaji China. China itaharakisha kujenga muundo mpya wa maendeleo wa mzunguko wa ndani kama nguzo kuu, na kuhimizana kwa mizunguko miwili ya ndani na kimataifa, kujenga mfumo wa hali ya juu wa uchumi wa soko la kijamaa, na kufungua mlango zaidi. Hii itatoa nafasi kubwa zaidi kwa maendeleo ya aina mbalimbali za makampuni.

Baada ya juhudi za zaidi ya miaka mia moja, Chama cha Kikomunisti cha China kimeanza safari mpya. Hii ni safari inayojaa utukufu na ndoto, na Wakomunisti watafanya kile wanachoahidi. Katika safari mpya ya kujenga nchi ya kisasa ya kijamaa kwa pande zote, Chama hicho na watu wa China kinaowaongoza wana imani na uwezo kamili wa kuanzisha mwujiza mpya na mkubwa zaidi utakaoshangaza dunia, ili kujiendeleza na kuleta manufaa zaidi kwa dunia!