Kenya yajiandaa na maonesho ili kuimarisha uhusiano kati ya China na Kenya
2022-10-25 08:53:41| CRI

Mkurugenzi mkuu wa Afripeak Expo Kenya, waandaji wa Maonesho ya tano ya Kimataifa ya Viwanda ya Kenya (KIIE) Bw. Gao Wei amesema maonyesho hayo yataimarisha uhusiano kati ya China na Kenya.

Gao ameeleza kuwa makampuni 130 kutoka China na mataifa mengine yataonyesha bidhaa zao kwenye maonyesho hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 mwezi ujao.

Banda la Kenya pia litachukua kampuni 20 za nchi hiyo ambazo zitaonyesha bidhaa zao na kutafuta wateja kutoka nje ya nchi.

Meneja mkuu anayesimamia ukuzaji wa uwekezaji katika Mamlaka ya Uwekezaji nchini Kenya Bw. Pius Rotich amesema kuwa maonyesho hayo yanatoa fursa kwa Kenya kuimarisha harakati zake za kukuza viwanda kupitia uhusiano na ushirikiano na kampuni za China. Bw.   Rotich alibainisha kuwa maonyesho hayo ni fursa nzuri kwa kampuni za Kenya kutafuta masoko mapya ya chai, kahawa, parachichi na maua nchini China.