UM wasema kumaliza vurugu za kijamii ni muhimu katika kupata amani endelevu nchini Sudan Kusini
2022-10-25 08:56:05| CRI

Naibu Mwakilisi Maalumu wa Tume ya Umoja wa Mataifa (UNMISS) na Mratibu Mkaazi nchini Sudan Kusini, Sara Beysolow Nyati amesema Sudan Kusini inapaswa kushughulikia kumaliza vurugu za kijamii zinazotokea kila baada ya muda katika ngazi za mitaa ili kupata maendeleo tulivu ya amani katika kipindi cha mpito kilichoongezwa.

Akiongea katika sherehe za kuadhimisha Siku ya Umoja wa Mataiafa huko Juba, Bi Nyati amezitaka pande zote za makubaliano mapya ya amani ya mwaka 2018, kukamilisha kazi muhimu ambazo hazijafanywa, kabla ya kumalizika kwa kipindi cha mpito mwezi Februari mwaka 2025. Amesema kuna kazi ambazo bado hazijatekelezwa katika ngazi za mitaa, na kuongezwa muda kwa makubaliano ya amani kunahitaji kutafsiriwa katika kupunguza matukio ya vurugu na migogoro kwenye ngazi ambayo haijafikia ya taifa.