Xi asisitiza kutekeleza kanuni elekezi za Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama katika vikosi vya jeshi
2022-10-25 09:05:16| CRI

Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Xi Jinping amevielekeza vikosi vya jeshi kujifunza, kutangaza na kutekeleza kanuni elekezi za Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, na kujitahidi kufikia lengo lililowekwa la karne la Jeshi la Ukombozi wa Umma (PLA).

Xi, ambaye pia ni rais na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi (CMC), aliyasema hayo alipohudhuria mkutano wa makada wakuu wa jeshi, ambapo amesisitiza kuwa katika miaka mitano tangu Mkutano Mkuu wa 19 wa CPC ufanyike mwaka 2017, CMC imeongoza vikosi vya jeshi kupata maendeleo makubwa na kutimiza mageuzi makubwa katika ulinzi wa taifa na jeshi. Pia amebainisha kuwa CMC imeshikilia uongozi imara wa Chama kwenye jeshi la umma, na kuimarisha na kupanua maendeleo ya kasi na mazuri katika njia ya kujenga jeshi imara, na kulifikisha jeshi la kisasa na uwezo wa kupambana katika ngazi ya juu.