AU yasaidia mazungumzo ya kumaliza mgogoro kaskazini mwa Ethiopia
2022-10-26 09:51:33| CRI

Umoja wa Afrika (AU) umewezesha mazungumzo ya moja kwa moja ya amani kati ya serikali ya Ethiopia na waasi wa Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) nchini Afrika Kusini.

Hatua hiyo ni sehemu ya mchakato unaoendelea wa Umoja wa Afrika kusaidia pande zenye mgogoro kaskazini mwa Ethiopia kupata suluhu ya kisiasa kwenye mgogoro wa mkoa wa Tigray. Mazungumzo hayo ya moja kwa moja yamewezeshwa na mwakilishi wa ngazi ya juu wa AU katika pembe ya Afrika na rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo pamoja na rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta, na naibu rais wa zamani wa Afrika Kusini Phumzile Mlambo-Ngcuka.

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ametiwa moyo na dhamira iliyooneshwa awali na pande husika ya kutaka amani na kutafuta suluhu ya kudumu ya kisiasa kwenye mgogoro kwa maslahi makuu ya Ethiopia.