Uongozi wa CPC waweka taratibu za kutekeleza kanuni elekezi za Mkutano Mkuu wa chama
2022-10-26 09:49:59| CRI

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ilikutana jana Jumanne ili kuweka taratibu za kujifunza, kutangaza na kutekeleza kanuni elekezi za Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC.

Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Xi Jinping, aliongoza mkutano huo, ambao pia ulijadili taratibu za kuimarisha na kulinda uongozi mkuu na wa umoja wa Kamati Kuu ya Chama na sheria za kina za utekelezaji wa maamuzi manane juu ya maadili ya kazi. Mkutano huo umebainisha kuwa kujifunza, kutangaza na kutekeleza kanuni elekezi za Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama ni kazi ya msingi ya kisiasa kwa Chama na nchi kwa hivi sasa na hata siku zijazo.

Aidha mkutano umetaka kuwepo uelewa wa kina juu ya umuhimu wa uamuzi wa kuanzishwa kwa nafasi kuu ya Komredi Xi Jinping katika Kamati Kuu ya chama na katika chama kwa jumla, na jukumu la uongozi la fikra ya Xi Jinping ya Ujamaa wenye umalumu wa China katika zama mpya.