Rais Ruto wa Kenya na katibu mkuu wa chama cha UDA wampongeza Xi Jinping kwa kuchaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC
2022-10-26 09:53:19| CRI

Kiongozi wa chama tawala cha Kenya UDA ambaye pia ni rais wa Kenya William Ruto ametuma barua ya kumpongeza Xi Jinping kwa kuchaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC.

Kwenye barua yake, rais Ruto akiwa kwa niaba ya watu wa Kenya na yeye mwenyewe, alisema Xi ametoa mfano wa kuigwa kwa kutoa kipaumbele maslahi ya wananchi na moyo wa kujitolea. Kenya inatarajia kushirikiana na China katika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya Afrika na China iliyo na uhai.

Naye katibu mkuu wa chama cha UDA Bibi Veronica Maina pia alituma barua ya pongezi kwa Xi Jinping akisema, chini ya uongozi wa Kamati Kuu ya CPC na katibu mkuu wake Xi Jinping, China imepata mafanikio makubwa yanayoshangaza dunia nzima. Anaamini kuwa mawasiliano kati ya vyama viwili yataweza kuendelea kuhimiza uhusiano kati ya nchi mbili uendelee vizuri kwa utulivu, na kutoa mchango katika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya Afrika na China yenye kiwango cha juu katika zama mpya.