Somalia aitaka EAC kuharakisha mchakato wa kuiingiza kwenye jumuiya
2022-10-27 11:17:32| CRI

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud ameitaka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuharakisha mchakato wa kuiingiza nchi hiyo kwenye Jumuiya hiyo na kuwa mwanachama wa 8.

Kwa mujibu wa taarifa ya EAC iliyotolewa Jumatano kwenye makao makuu yake mjini Arusha Tanzania, rais Muhamud ametoa wito huo wakati Katibu mkuu wa EAC Peter Mathuki alipotembelea kwa mara ya kwanza Mogadishu nchini Somalia. Muhamud amesema nchi yake kujiunga na Jumuiya hiyo imekuwa ndoto inayocheleweshwa kwa serikali ya Somalia na watu wake.

Jumuiya ya Afrika Mashariki inaundwa na nchi kama vile Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda.