Afrika Mashariki kuharakisha uoanishaji wa viwango vya chakula ili kuongeza kasi ya biashara ndani ya kanda
2022-10-27 11:16:59| CRI

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinaharakisha kuoanisha viwango vya chakula ili kuongeza kasi ya biashara ndani ya kanda.

Akiongea mjini Nairobi Kenya, mkuu wa usalama wa chakula katika Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Kenya Mary Mwale, amesema kanda hiyo imekubaliana kuongeza ushirikiano na kutumia mbinu za pamoja katika kutambua kwa pamoja viwango vya usalama katika vituo vya mpakani.

Naye mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ya Tanzania Frank Mmbando amesema hatua sawa za usalama wa chakula katika jumuiya ya EAC zitaongeza ushindani wa bidhaa za biashara za kilimo ndani na nje ya kanda, na kusema uainisho pia utasaidia kukabiliana na magonjwa ya wanyama ya kuvuka mipaka, pamoja na kukabiliana na tatizo la udhaifu wa kutambua na kufuatilia wanyama ambalo linaathiri mtiririko wa biashara ya kuvuka mipaka.

Kwa upande wa Mathilda Mukasekeru, kaimu mkurugenzi wa Maendeleo ya Rasilimali za Wanyama kwenye Wizara ya Kilimo na rasilimali za wanyama ya Rwanda amesema sekta ya kilimo ya EAC inakabiliwa na changamoto zinazofanana za usalama wa chakula.