Rais Xi afanya ziara mikoani Shaanxi na Henan asisitiza ufufuaji wa vijiji
2022-10-29 15:00:56| cri

 

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuendeleza kazi ufufuaji wa vijiji kote nchini na kufanya juhudi bila kuchoka ili kufikia kilimo na kisasa vijijini.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya ukaguzi mjini Yan'an, Mkoani Shaanxi, na mjini Anyang mkoani Henan, kwenye ziara alizofanya kuanzia Jumatano hadi Ijumaa.

Akiongea na wanakijiji katika shamba moja la matunda, Rais Xi aliwauliza kuhusu shughuli zao za kilimo, tangu upandaji, biashara na faida. Rais Xi alifahamishwa kuhusu maendeleo ya jumla ya kilima cha matufaha katika eneo hilo. Rais Xi alikumbusha kuwa aliishi kaskazini mwa Shaanxi kwa muda wa miaka saba, na kuona wanakijiji wakiishi katika hali ngumu, na aliendelea kufikiria njia za kufanya maisha yao kuwa bora.

Rais Xi pia alitembelea shule ya sekondari ya Yan'an ambako alielezea matumaini kuwa shule hiyo itadumisha Roho ya Yan'an wakati wa kutoa ujuzi na kuendeleza maadili. Akiwa darasani, Rais Xi aliwauliza wanafunzi kuhusu maadili yao na wanachotaka kufanya watakapokuwa wakubwa. Rais Xi aliwahimiza wanafunzi hao kuweka malengo makubwa mapema na kutamani kuchangia na kuendeleza kazi ya ujamaa.