Rais wa China atoa salamu za pole kwa rais wa Korea Kusini kutokana janga lililotokana na tukio la kukanyagana nchini humo
2022-10-30 18:28:45| CRI

Rais Xi Jinping wa China amemtumia salamu za pole rais Yoon Suk-yeol wa Korea Kusini kutokana na tukio la kukanyagana lililotokea huko Seoul, mji mkuu wa Korea Kusini lililosababisha vifo na majeruhi wengi.

Kwenye salamu hizo, rais Xi, kwa niaba ya serikali na watu wa China, ametoa salamu za pole kwa wafiwa na familia zao.

Amesema raia kadhaa wa China pia wamefariki katika tukio hilo, na anatumai Korea Kusini itafanya uokoaji na kupanga vizuri shughuli zinazohusika kadiri iwezavyo.