Xi Jinping apongeza miaka 65 ya kuanzishwa kwa Shirika la Urafiki wa Russia na China
2022-10-31 13:10:30| CRI

Rais Xi Jinping wa China tarehe 29 alituma salamu za pongezi za kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa  Shirika la Urafiki wa Russia na China.

Rais Xi amesema shirika hilo limekuwa likishika mtazamo wa kuwa na urafiki na China tangu lianzishwe miaka 65 iliyopita, na kutoa mchango muhimu kwa ajili ya maelewano, urafiki, uaminifu kati ya watu, na kuimarisha msingi wa maoni ya umma wa uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili. Ameeleza matumaini yake kuwa Shirika   la Urafiki wa Russia na China litaendelea kuenzi desturi bora na kufanya kazi kubwa zaidi kwa ajili ya maelewano kati ya watu wa China na Russia.

Siku hiyo, rais Vladimir Putin wa Russia naye pia alituma salamu za pongezi tangu Shirika  hilo lianzishwe miaka 65 iliyopita.