Watu 153 wafariki na wengine kujeruhiwa katika tukio la kukanyagana nchini Korea Kusini
2022-10-31 08:45:41| CRI

Watu 153 wamefariki na wengine 103 kujeruhiwa katika tulio la kukanyagana lililotokea jumamosi usiku katika wilaya ya Itaewon, pembezoni mwa mji wa Seoul, wakati watu walipokusanyika kusherehekea Sikukuu ya Halloween.

Uchochoro huo wenye ukubwa wa mita sita, ulijaa kupita kiasi kutokana na watu waliokwenda kufurahia sikukuu hiyo, ambao walikuwa wakitembelea migahawa na baa katika eneo hilo.

Hili ni janga baya zaidi kutokea nchini humo tangu kuzama kwa kivuko mwezi April, 2014, ambapo watu 304 walifariki katika ajali hiyo.