Xi Jinping: ziara ya Nguyen Phu Trong imeonyesha kutilia maanani kukuza uhusiano wa vyama vya China na Vietnam
2022-10-31 21:43:06| CRI

Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na rais wa China Xi Jinping leo hapa Beijing amekutana na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam CPV Nguyen Phu Trong.

Kwenye mazungumzo yao, Xi Jinping alisema Katibu Mkuu Nguyen Phu Trong ni kiongozi wa kwanza wa nchi ya nje kukutana naye baada ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, na hii pia ni ziara ya kwanza Nguyen Phu Trongnje anayofanya nje ya nchi baada ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa 13 wa CPV, jambo ambalo limeonyesha vya kutosha kuwa wao wanatilia maanani sana kukuza uhusiano wa nchi na vyama vya China na Vietnam. Xi alisema anapenda kubadilishana maoni kwa kina juu ya ujenzi wa ujamaa wa China na Vietnam, na maendeleo ya uhusiano wa nchi na vyama vya nchi hizo mbili.

Naye Nguyen Phu Trong alisema amefuata ahadi yake kuwa kama hali inakubalika, China itakuwa nchi yake ya kwanza kutembelea baada ya kuchaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa kamati kuu ya CPV mwezi Januari mwaka 2021. Amepongeza kufanyika kwa mafanikio Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC kwa niaba ya chama cha CPV na nchi ya Vietnam na wananchi wake, akisema mafanikio hayo yameonesha kuwa katika miaka kumi iliyopita, Fikra ya Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye Umaalum wa China imetoa mchango mkubwa wa uongozi katika kuongoza Chama, nchi na watu kutimiza maendeleo makubwa pamoja na uungaji mkono mkubwa kwa heshima ya komradi Xi Jinping kimataifa.