Idadi ya vifo vilivyotokana na kubomoka kwa daraja nchini India yafikia 60
2022-10-31 08:47:15| CRI

Idadi ya vifo vilivyosababishwa na kuanguka kwa daraja katika Jimbo la Gujarat magharibi mwa India imeongezeka na kufikia 60 mpaka jana Jumapili.

Kazi ya uokoaji inaendelea, ingawa watu wengi bado wamekwama kwenye mto baada ya daraja hilo kuanguka.

Gazeti la Tribune limeripoti kuwa, daraja hilo limefunguliwa tena kwa umma siku nne baada ya kazi ya ukarabati kukamilika.

Waziri mkuu wa India Narendra Modi amezungumza na maafisa wa serikali ya Jimbo hilo na kuwaelekeza kutoa msaada kwa waathirika.

Serikali ya jimbo hilo imetangaza kutoa fidia ya Rupia laki nne, sawa na dola za kimarekani 4,860, kwa kila familia ya waliofariki. 

Pia, waziri mkuu Modi ametoa fidia ya Rupia laki mbili, sawa na dola za kimarekani 2,430 kutoka Mfuko wa Taifa wa Usaidizi wa Waziri Mkuu kwa kila familia iliyofiwa.