Xi jinping apongeza kufanyika kwa mkutano wa pili wa dunia wa maendeleo endelevu ya miji
2022-10-31 16:35:06| CRI

Rais Xi Jinping wa China leo ametuma salamu za pongezi kwa kufanyika kwa shughuli ya kuadhimisha Siku ya Miji Duniani na mkutano wa pili wa dunia wa maendeleo endelevu ya miji kwa mwaka 2022 mjini Shanghai, China.

Rais Xi amesema shughuli hiyo inafanyika chini ya wazo la “Miji, Inafanya Maisha kuwa Bora zaidi” inalenga kuhimiza maendeleo endelevu ya miji duniani, na ina umuhimu mkubwa kwa maendeleo yenye uwiano, jumuishi, uratibu na masikilizano, ushirikiano na mafanikio kwa pamoja na ustawi wa pamoja. Ameeleza matumaini yake kuwa miji ya nchi mbalimbali itajiunga na pendekezo la maendeleo duniani, kuongeza kasi ya kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa na “Ajenda Mpya ya Miji”, kuchangia ukuaji wa uchumi, kuboresha mazingira ya ikolojia, kuinua uwezo wa kusimamia miji na kuhimiza maendeleo endelevu ya dunia.