Rais wa China atoa salamu za pole kwa rais wa India kutokana na kubomoka kwa daraja nchini humo
2022-11-01 19:49:41| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pole kwa rais Droupadi Murmu wa India na waziri mkuu wa nchi hiyo Narendra Modi kutokana na ajali ya kubomoka kwa daraja iliyotokea kwenye Jimbo la Gujarat nchini humo ambayo imesababisha vifo na majeruhi wengi.

Kwenye salamu hizo, rais Xi, kwa niaba ya serikali na watu wa China, ametoa salamu za pole kwa familia za wafiwa.