Mjumbe wa Umoja wa Afrika atoa wito wa kusimamisha vita nchini DRC
2022-11-01 08:56:28| CRI

Mjumbe wa amani wa Umoja wa Afrika, Uhuru Kenyatta, ametoa wito wa kusimamisha mapambano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambayo yamesababisha vifo vya watu na uharibifu wa mali, na watu wengi kukimbia makazi yao.

Kenyatta, ambaye ni rais wa zamani wa Kenya na mjumbe wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu mazungumzo ya ndani ya DRC na kurejesha amani na utulivu mashariki mwa nchi hiyo, amesema anasikitishwa na kuongezeka kwa migogoro ya kibinadamu kwenye eneo hilo. Ametoa wito kwa pande zinazohusika kusitisha mara moja vitendo vya chuki, kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia walengwa, kuondoka kutoka maeneo yanayokaliwa kwa mabavu, na kutafuta suluhu kupitia mazungumzo ya amani.