Mradi wa kuondoa umasikini kuwanufaisha watu wa vijijini nchini Zambia
2022-11-01 08:54:04| CRI

Mradi wa kuondokana na umasikini unaofadhiliwa na China unalenga kuwasaidia wanavijiji katika maeneo ya ndani nchini Zambia kuongeza uzalishaji wa kilimo na kuongeza kipato chao.

Mradi huo unaoitwa Kijiji cha Mfano cha Maendeleo ya Kilimo ya China na Afrika na Kupunguza Umasikini, ulipendekezwa katika Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika mwezi Novemba mwaka jana, utawezesha kuanzishwa kwa vijiji vya mfano katika maeneo ya vijijini nchini Zambia katika miaka michache ijayo.

Mapema mwezi uliopita, kijiji cha mfano kilianzishwa katika Kijiji cha Shimwengwe wilaya ya Chongwe, mkoa wa Lusaka, ambapo kupitia mradi huo, wanakijiji watawezeshwa kwa elimu na teknolojia ndogo ili kuboresha uzalishaji katika biashara ya ufugaji wa kuku.

Mratibu wa mradi huo, Simushi Liswaniso, amesema mradi huo, ambao umeanzishwa mwaka huu na utaendelea hadi mwaka 2025, na kuishukuru serikali ya China kwa kuunga mkono mradi huo, na kuongeza kuwa miradi kama hiyo itaimarisha urafiki kati ya nchi hizo mbili kwa kuwa inalenga kuboresha maisha ya watu.