Idadi ya vifo katika ajali ya daraja nchini India yaongezeka hadi 132
2022-11-01 09:23:15| CRI

Waziri wa Mambo ya Ndani wa jimbo la Gujarat nchini India, Hash Sanghawi, amesema idadi ya watu waliofariki katika ajali ya kuanguka kwa daraja katika jimbo hilo imeongezeka hadi 132, na kazi ya uokoaji inaendelea.

Kutokana na ripoti za vyombo vya habari vya India, daraja la juu la waenda kwa miguu katika jimbo la magharibi mwa India la Gujarat lilianguka ghafla tarehe 30, na watu wengi wakiwemo wanawake na watoto waliangukia mtoni. Afisa wa jimbo hilo alisema huenda daraja hilo lilianguka kutokana na kubeba watu wengi kupita kiasi.