Wataalam wa hali ya hewa wa Afrika kuhimiza upatikanaji wa fedha katika mkutano wa COP27
2022-11-02 08:43:14| CRI

Wataalam wa Afrika katika mkutano ujao wa 27 wa Nchi Zilizosaini Makubaliano ya Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP27) utakaofanyika Sharm-el-Sheikh nchini Misri, watahimiza kutolewa kipaumbele kwa mahitaji ya bara hilo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi wakati hasara na madhara yanayotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi vikiongezeka.

Wataalam hao kutoka Shirika la Maendeleo ya Serikali za Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) wamesema katika taarifa yao iliyotolewa jana mjini Nairobi, kenya, kuwa nchi zilizoendelea zinatoa kiasi kikubwa cha hewa chafu na kusababisha mabadiliko ya tabianchi, hivyo zinapaswa kutoa fedha ili kusaidia hatua za udhibiti zinazochukuliwa na nchi zinazoendelea ambazo zinaathirika zaidi kwa kuwa hazikujiandaa kukabiliana na hali hiyo.

Mkurugenzi wa Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa na Ongezeko la Joto kilicho chini ya IGAD (ICPAC) Guleid Artan amesema, Afrika inataitaka dunia kutambua kuwa inabeba mzigo mkubwa wa athari za mabadiliko ya tabianchi.