Maonyesho ya 5 ya CIIE yavutia nchi, maeneo na mashirika ya kimataifa 145
2022-11-02 08:43:28| cri

Jumla ya nchi, maeneo na mashirika ya kimataifa 145 yatashiriki katika Maonesho ya 5 ya Kimataifa ya Uagizaji wa Bidhaa ya China, (CIIE), ikiwa ni pamoja na kampuni 284 zinazoshika nafasi 500 za mwanzo duniani.

Kwa mujibu wa naibu mkurugenzi wa Idara ya Maonyesho hayo Bw. Sun Chenghai, kampuni kutoka nchi na maeneo 127 zitashiriki katika maonyesho ya biashara na viwanda, na nchi 66 na mashirika matatu ya kimataifa yatashiriki kwenye maonyesho ya kitaifa, ikiwa ni idadi kubwa zaidi kuliko ile ya mwaka jana.