Mradi wa Africa CDC ni ushahidi mwingine wa zawadi ya China kwa Afrika
2022-11-02 08:42:21| CRI

Aliyekuwa Balozi wa Ethiopia katika Umoja wa Mataifa Teruneh Zenna amesema, ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) utakuwa ni zawadi nyingine ya China kwa Afrika.

Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China hivi karibuni, Balozi Zenna amesema, serikali ya China sio tu imefadhili bali pia inajenga makao makuu ya Africa CDC ambayo yatakusanya ofisi zote katika sehemu moja ili kuboresha mfumo wa afya barani Afrika.

Amesema bara la Afrika linakosa maandalizi na taasisi za afya zinazoweza kukabiliana na milipuko ya mgonjwa kama Ebola na UKIMWI, jambo lililosababisha vifo vya watu wengi barani humo, na kusema kuwa na taasisi kama hiyo katika ardhi ya Afrika ni jambo la kusifiwa.

Ameongeza kuwa, kutumia Makao Makuu hayo kama kamandi kuu, Umoja wa Afrika utasaidia nchi wanachama wake kuimarisha uwezo wao wa kugundua na kujibu kwa haraka na kwa ufanisi matishio na milipuko ya magonjwa kama Ebola, COVID-19 na homa ya manjano.