China yaitaka serikali ya Somalia itekeleze kihalisi majukumu ya kulinda amani na usalama wa taifa
2022-11-02 08:47:33| CRI

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing hivi karibuni alisema, China inaitaka serikali ya Somalia itekeleze kihalisi majukumu ya kulinda amani na usalama wa taifa.

Balozi Dai amesema, China pia inaitaka serikali ya Somalia ifanye juhudi zaidi katika kuboresha suala la mgogoro wa kibinadamu, na kuendelea kuimarisha udhibiti wa silaha. Amesema kama Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litarekebisha vikwazo dhidi ya Somalia, ni lazima serikali ya Somlia iongeze uwezo wa udhibiti wa silaha.