Wanawake wanavyojikwamua kiuchumi na changamoto wanazokumbana nazo
2022-11-04 08:00:19| CRI

Wanawake ni kundi kubwa ama naweza kusema ni jeshi kubwa, na wanapoamua kufanya jambo lao, ni wazi kuwa mafanikio ni Dhahiri. Iwe ni katika nyanja za siasa, kijamii, uongozi, biashara, sayansi na teknolojia, ufundi, na Nyanja nyingine zozote, mwanamke akiamua, hakika anaweza.

Vipindi vilivyopita tulizungumzia kuhusu wanawake wanaofanya kazi ambazo awali ilidhaniwa kuwa ni wanaume pekee ndio wanaweza kufanya, na hata pia tumezungumzia wanawake katika sekta ya sayansi na teknolojia na pia katika uongozi. Tumeona jinsi wanawake wanavyobadili mawazo ya zamani kwamba nafasi ya mwanamke ni jikoni na kulea familia, na sasa wameingia katika kufanya kazi sawa ama hata zaidi ya wanavyofanya wanaume.

Kwa mfano katika kipindi kilichopita tuliona jinsi wanawake wanavyojitahidi kupenya katika masuala ya kisiasa, ingawa bado hawajapata nafasi zaidi, lakini juhudi zao zinaonekana na kupongezwa na jamii. Katika kipindi cha leo tutazungumzia jinsi wanawake wanavyojitahidi kuondokana na utegemezi kwa waume zao na kutafuta njia za kujiingizia kipato kwa kufanya shughuli mbalimbali, lakini pia tutazungumzia changamoto wanazokumbana nazo katika kujiinua kiuchumi.