Mkutano wa AL wamalizika kwa kutoa wito wa juhudi za pamoja kukabiliana na changamoto mbalimbali
2022-11-03 08:33:31| CRI

Mkutano wa 31 wa Umoja wa Nchi za Kiarabu (AL) umemalizika jana jumatano kwa kupitisha Azimio la Algiers linalotoa wito wa juhudi za pamoja kukabiliana na changamoto za kikanda na kimataifa.

Azimio hilo limeonya kuhusu hatari zinazoletwa na kubadilika kwa mazingira ya kimataifa katika usalama na utulivu wa nchi za Kiarabu, na kusisitiza umuhimu wa kuunganisha juhudi za pamoja ili kulinda maslahi ya nchi hizo.

Pia azimio hilo limetoa wito wa ushirikiano katika kuhakikisha usalama wa chakula na nishati, kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, na pia kumaliza migogoro katika baadhi ya nchi za Kiarabu.