China yatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kujitahidi kuhakikisha kila mkimbizi analindwa
2022-11-03 08:33:26| cri

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Geng Shuang amesema, China itaendelea kuunga mkono kazi za Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) na Kamishna Mkuu wa Shirika hilo, na kwamba jumuiya ya kimataifa inapaswa kuongeza juhudi za kutoa misaada ili kuhakikisha kila mkimbizi analindwa.

Balozi Geng amesema, mwaka huu, idadi ya jumla ya wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao duniani imezidi milioni 100 kwa mara ya kwanza, na mahitaji ya kibinadamu ya kundi hili yameongezeka, wakati ufadhili wa kibinadamu kwa ajili yao hautoshi, na hivyo kulazimisha mashirika ya kibinadamu kupunguza viwango vya misaada.

Balozi Geng pia amesema, nchi zinazoendelea zimepokea asilimia 83 ya wakimbizi duniani, na nchi zilizoendelea zinapaswa kutimiza kwa dhati ahadi zao za kusaidia nchi zinazoendelea kupunguza shinikizo hilo.