Kenya yapeleka askari wa kulinda amani nchini DRC
2022-11-03 08:34:22| CRI

Rais wa Kenya William Ruto jana jumatano amewaaga askari wa Kenya wanaokwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kutekeleza jukumu la ulinzi wa amani.

Akiwaaga askari hao, rais Ruto amesema kikosi hicho kitakwenda mashariki mwa DRC na kitafanya kazi chini ya uongozi wa Kikosi cha Ulinzi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF). Amesema DRC imepata mafanikio makubwa katika kutuliza na kujenga uwezo wa kitaifa kutoa huduma za usalama na pia kuhakikisha fursa mbalimbali kwa ajili ya wananchi wa nchi hiyo.

Kupelekwa kwa askari wa Kenya nchini DRC kunafuatia uamuzi uliopitishwa na viongozi wa kikanda katika Mkutano wa Tatu wa Faragha wa Wakuu wa EAC kuhusu Amani na Usalama mashariki mwa DRC uliofanyika mwezi Juni jijini Nairobi, Kenya.